Walimu na Wakufunz

WANAFUNZI WETU WAHAMIAJI NI AKINA NANI?

Familia za uhamiaji zinayostahiki kuhudumiwa katika bonde la Shenandoah ni familia zilizohamia katika kipindi cha miaka 3 zilizopita wakiwa wanatafuta kazi katika kilimo au usindikaji wa chakula mbichi. Familia zilizopanuliwa au watu kutoka mji moja hupatikana wakiwa karibu, kutoa uungaji mkono na kusaidiana. Ni muhumu kutambua kwamba wahamiaji wote siyo Wahispania, kama vile Wahispania wote siyo wahamiaji. Wakati jumla ya wanafunzi na wazazi wahamiaji ni Wahispania, kuna idadi ya familia wahamiaji iinayoongezeka kutoka Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati. Wanafunzi wetu na familia wanakuwa na asili toufauti katika utamaduni, mila, na elimu. Tunawahudumia wanafunzi na familia zetu na thamani kubwa ya mafanikio katika elimu, ajira, na fursa za mbele.

MWALIMU MKUFUNZI WA KUJITOLEA KWA ELIMU YA UHAMIAJI

Mpango wa Elimu ya Wahamiaji inategemea timu ya walimu wakufunzi wa kujitolea kutoa elimu sehemu za nyumbani na madarasani ya wanafunzi wahamiaji wenye umri ya kusoma. Wenye kujitolea wanakutana na wanafunzi wao mara mbili kwa wiki kwa vipindi vya mafunzo vinavyochukua lisaa limoja. Walimu wakufunzi wanatumia muda huu kuwasaidia wanafunzi na mazoezi ya nyumbani; walakini, pia wanakaribishwa kuandaa shughuli, michezo, na masomo kwa wanafunzi wao. Walimu wakufunzi wanakuwa kama rasilimali ya elimu kwa wanafunzi wahamiaji—wanawasaidia na kazi za shule na kuwasaidia waendeleze ustadi wao na kujiamini na kufikia malengo yay a kitaaluma. Wanaojitolea ni washauri pia, wanakuza mapendo ya kujifunza na wanaonyesha chaguzi bora na usalama wa maisha kutokana na mifano yao. Wanaojitolea na Mpango wa Elimu ya Wahamiaji (Migrant Education Program) wanalipwa na nafasi ya kuingia katika mawasiliano, lugha, na ustadi wa kufundisha, na wanapata marafiki wa kuduma kwa maisha katika jamii yao. Mtu yeyote anayetamini kuleta mabadilisho mazuri katika maisha ya mwanafunzi mhamiaji anakaribishwa kuomba hiyo kazi – hakuna uzoefu wa kufundisha au kusema lugha ya kigeni unaohitajika. Kuajiri na mafunzo yanatokea kila mwezi wa Septemba na mwezi wa Januari. Ikiwa una nia ya kujitolea katika mpango wetu tafadhali pakua ombi na irudishe kwa njia ya barua pepe kwa shenvalleymigranted@jmu.edu.

Ombi la Mwalimu Mkufunzi (Word)

WANAFUNZI WAHAMIAJI WANAFUZU VIPI KUPOKEA HUDUMA

Wafanyakazi wa Elimu ya Wahamiaji wanatoa maswali ya kustahiki kwa kila shule katika mkoa wa huduma kwa kuingizwa katika pakiti wa uandikishaji. Wakati familia wanawaandikisha watoto wao kuingia shuleni, wanajaza fomu ya kustahiki. Halafu, shule zinazirudisha fomu za maswali zilizokamilishwa ofisini ya Elimu wa Wahamiaji, ambapo wafanyakazi wa SVMEP wanazikagua kuamua ustahiki wa kila familia. Kisha wafanyakazi wa SVMEP wanafanya mahojiano kwa simu na mzazi au mlezi wa mtoto wa kila mwanafunzi mhamiaji anayeweza kustahikiwa. Kama kuna ushahidi wa kutosha wa ustahiki wake wa mwanafunzi kwa mpango ya Elimu ya Wahamiaji wakati wa mahojiano kwa njia ya simu, kisha ziara ya nyumbani inapangwa na familia kukamilisha fomu zao za kuandikishwa na kuwapa taarifa zingine kuhusu SVMEP na huduma zake. Pamoja na kushirikiana sana na shule za umma katika mkoa wetu wa huduma, SVMEP pia inasambaza wauzaji katika vitongoji vwenye idadi ya wahamiaji wengi.  SVMEP inatembelea viwanda vya kuku kila wiki mbili, na kila mwaka inatembelea shamba za matunda ili kutambua na kuajjiri mwanafunzi mpia.

ELIMU YA WAHAMIAJI INASAIDIAJE WANAFUNZI NA KUUNGAJE WAFANYAKAZI?

Elimu ya wahamiaji inatoa utetezi na huduma za mafunzo nyongeza kwa wanafunzi wenye umri wa kustahiki kusoma chekechea na shule, pamoja na vijana chini ya umri wa miaka 22, kulenga wanafunzi walio hatarini kutokana na hali ya kuhamia sana na/au ustadi mdogo wa Kiingereza.

Kuwahudumia walimu, Migrant Education inaweza ku:

  • Kutoa wakufunzi kwa wanafunzi wanaohitaji msaada wa ziada wenye kitaaluma.
  • Kuwashauri vijana mpaka wamalize shule sekondari na mpaka uanzishwaji wa malengo ya baadaye ya elimu na kazi
  • Kuhimiza ushiriki wa mzazi kwa njia ya ziara ya nyumbani na msaada na mikutano baina ya walimu na wazazi, ya vikao vya wazazi.
  • Kupanga, kusafirisha, na kutafsiri kwa miadi zinaoathiri elimu au ustawi wa mtoto
  • Kutoa mafunzo ya kusoma na kuandika kwa njia ya ziara ya nyumbani ya familia zinazokuwa na watoto wenye umri wa chekechea